1

4 0 0
                                    

Sumaku.Chini ya uongozi wa Rais Mheshimiwa mteule ilikuwa inatazamia kuadhimisha miaka hamsini Na sita tangu Uhuru.Uhuru ambao wananchi hawajui washerehekee au wakashifu.

Wanasumaku wanaandamwa Na shida mbalimbali huku serikali ikiwahidi kushughulikia mahitaji yao.

Kinacgofuata ni simanzi wananchi wakifa njaa,wafanyikazi wakigoma kila kuchao,mafuriko yakisomba watu,ufisadi uliokithiri,siasa zisizojenga nchi,maandamano na vifo.

Serikali ya Sumaku inawafunga wezi wa kuku na vifaranga huku wafisadi waliopora mali ya umma wakiongezewa walinzi zaidi.

Maandalizi ya sherehe za Siku kuu ya Uhuru Sumaku yakiendelea nchi inakumbwa na changamoto ambazo haziangaziwi hata kwa vyombo vya habari.

Wanaoipinga serikali wanaangushwa na mtutu wa bunduki huku walio vibaraka wanapewa vyeo serikalini.

Sumaku kweli ni nchi bora barani na hivyo wananchi wanafaa kujivunia.

Serikali inawashughulikia maiti zaidi ya walio hai na "gharama" ya mazishi inagharamiwa.....

Ndio nchi bora hii ya mamilionea wachache zaidi...

Hadithi imeanza tuu....na itaendelea....

SUMAKU Où les histoires vivent. Découvrez maintenant