Sura ya Tisa

22 1 0
                                    

Maria alipomaliza kidato cha nne alijiunga na chuo kimoja  mjini kwao Nairobi, kusomea Ulimbwende.
Ni masomo aliyoazimia tangu utotoni.
Akiwa kule chuoni alishiriki mashindano kadhaa ya mavazi na urembo.
Maria alikuwa ni tausi.
Alipokanyaga safakuni,kifua mbele na kichwa juu, kwake ilikuwa kazi rahisi isiyohitaji kiwewe wala wasiwasi.
Alikuwa na uwezo wa kuzaliwa nao wa miondoko na kuposi kwa picha kuliko washangaza wengi.
Kwake jukwaa la maonyesho likawa kama kidimbwi cha maji kwa samaki.
Aliwahi kuzipamba kurasa za majalida na magazeti mbali mbali.
Kimo chake kirefu na tabasamu la kukata na shoka lilimweka kwenye nafasi ya mbele zaidi ikilinganishwa na wapinzani wake.
Marie akawa kipenzi cha wasanii wa mavazi na urembo.
Nyota yake ilikuwa iking'aa ila moyoni hakuwa na amani.
Kuna mambo kadha yaliyomnyima lepe la usingizi.
Sekta ya Ulimbwende haikuwa imekubalika kabisa katika nchi yake.
Washiriki wa maonyesho kama yeye, walichukuliwa kama watu walegevu kimaadili na jamii.
Licha ya kuwa kuna nazi mbovu zilizowaaribia sifa wale wenye misimamo dhabiti kama Marie,kwake yeye ilikuwa ni kichumia uchumi kama kazi nyingine yeyote ile.
Wamiliki wa ajenti na kampuni za urembo waliwaona vipusa waliowasajiri kama windo rahisi la kukidhi kiu chao cha mapenzi.
Kwa wengi wao,kigezo cha kwanza kuingizwa kwenye kandarasi kilikuwa ujuzi wa kitandani.
Marie hakuwa yule Maria wa enzi za Pingoni.
Alikuwa na msimamo dhabiti na ukakamavu wa kufanikiwa katika nyanja hii.
Marie alikuwa mwenye azma ya kukwea ngazi na kushiriki majukwaa ya kimataifa.
Hatima yake ikiwa ni kuanzisha mitindo yake ya mavazi na kushiriki katika matangazo ya kibiashara.
Presha ya kuasi msimamo wake ilipomzidi,Marie aliamua kuwa mshiriki huru chini ya meneja wake wa kibinafsi.
Meneja wake akawa ni yule yule Nyundo waliosomea naye Mkiritini.
Kwa Marie ikawa ni afueni iliyomwezesha kuheshimika na kuiepuka mitego ya midume iliyojificha kwenye sekta hii kuwatumia mabinti wa watu kwa njia mbovu.
Kisa kati yake na Muktar;jamaa aliyeogopewa kakita sekta hii kilimfanya kukakata kauli ya kujisimamia yeye mwenyewe.
Muktar alikuwa na mazoea ya kuwanyakua warembo wabichi katika ajenti yake,kuwatumia na kisha kuwatupilia mbali.
Hakuna aliyedhubutu kumukashifu au kumshtaki.
Sekta ya Ulimbwende ilikuwa ni yeye na yeye alikuwa sekta ya Ulimbwende.
Muktar alishikilia sekta hii katika viganja vyake vya mikono.
Alikuwa na mifedha iliyomwezesha kumnyamazisha mpinzani yeyote na ushawishi mkubwa kakika vyombo vya usalama na mashirika ya habari.
Kwenda kumshtaki ilikuwa kama kujaribu kuukwea mlima  Kilimanjaro bila vifaa vyovyote.

Muktar alikuwa amemumulika  Marie kwa kurunzi  na kumwalika katika hoteli moja ya kifahari kujadiliana kuhusu kumsajiri katika kampuni yake maarufu.
Alimtuma mmoja wa wafanyikazi mtambuzi na mkuzaji wa vipawa kumpa Marie mwaliko.
"The boss is interested in your talent na anaomba mkutane katika mkahawa wa Zigizagi to discuss terms and sign the contract" Yolanda alimwarifu Marie.
Mkutano ulikuwa umepangwa Ijumaa hiyo na Muktar angempigia Marie kumpa maeleza zaidi.
"One more thing,Boss amesema husiandamane na mtu mwingine" Yolanda alihimiza.
"Haya usemavyo nitangoja simu yake!" Marie alisema kwa shauku.
Zigizagi ni mkahawa uliokuwa maarufu na uliotembelewa na matajiri,wafanyibiashara,viongozi na wageni maarufu nchini.
Mkahawa uliokuwa chini ya ulinzi mkali katika eneo tengwa mjini Nairobi.
Ni mkahawa uliokuwa pahali pa kawaida kwa Mubabe,babake Maria,kufanyia mikutano ya kisiasa na kibiashara.
Maria alikusudia kumwarifu babake kuhusu mkutano ule ili amsubiri waandamane kurudi nyumbani pamoja.
Muktar na Mubabe walifahamikiana kibiashara na aliifahamu fika kuwa Marie alikuwa mboni ya macho ya Mubabe,akiwa mtoto wa kipekee na wa kike.
Alikusudia kumtumia Maria ili kumkejeli na kumugadhabisha Mubabe.

**********************************
Simu iliingia Ijumaa hiyo asubuhi mwendo wa saa kumi na moja asubuhi.
"Hello,Muktar hapa,unayakumbuka mazungumzo yako na Yolanda mwanzoni mwa wiki?"
"Naam, nakumbuka bayana!" Marie alijibu.
"Vizuri naomba tukutane Zigizagi saa kumi na moja jioni,kwenye chumba cha mankuli cha twiga" Muktar alitoa mwaliko.
Marie hakukawia kumfahamisha babake kuhusu mwaliko huu.
Ilipofikia mwendo wa saa kumi,Marie alichukua gari lililotumwa na Muktar na kuelekea kwenye mahojiano.
Alivaa rinda nyekundu lililojimwayamwaya sakafuni na kumbidi kuliinua kwa mikono yake ili aweze kutembea.
Liliacha mpasuko upande wa kushoto uliofikia gotini.
Alipendeza na kuonekana kama malkia hasa kwa kuvalia bangili na viatu vilivorandana rangi na rinda lake.
Rinda hili alilibuni yeye mwenyewe pamoja na pochi aliyoibeba mkononi.
Kiwiliwili chake kirefu kilimfanya kuonekana kama malkia wa warembo wote duniani.
Saa kumi na moja Marie aliwasili katika hoteli ya Zigizagi na kulakiwa na mhudumu aliyempeleka moja kwa moja hadi kwenye chumba alichokuwa akimngoja Muktar.
Alopoingia chumbani alikumbana na mpiga picha maarufu wa kupiga picha za Ulimbwende.
Marie alipiga posi mlangoni,na kwingineko alikohitajika kabla ya kuketi kwenye meza alikokaribishwa kwa taadhima na Muktar.
Marie aliifahamu fika kuwa kuonekana kwake kwenye majarida akiwa na Muktar kungempandisha hadhi kigafla.
Alichokuwa hakijui Muktar,ni kuwa mhudumu aliyekuwa akiwashughulikia pale alikuwa amepewa maagizo maalum na Mubabe kuyanasa yote yaliyokuwa yakiendelea pale na kumwarifu mara moja endapo pangezuka hali yoyote ya mshikemshike.
Tayari kamera za siri kunasa picha na sauti zikuwa zimebandikwa mezani walikokaa Marie na Muktar.
"Pongezi kwa kuibuka chipukizi mwenye matumaini zaidi katika mashindano ya "upcoming beauty queens yaliyofanyika hivi majuzi"
"Na unapendeza kwelikweli" Muktar alimsifu huku akiupiga mkono wake busu na kumwinamia kama kitwana kwa malkia.
"Shukrani, namshkuru Maulana" alijibu Marie huku akilivuta rinda lake chini aweze kuketi bila usumbufu.
Walikula na kunywa vinywaji vyao na kuyazungumzia mambo mengi katika sekta hii yao.
Muktar alimwelezea Marie kwa kirefu kuhusu shindano ambalo angeliandaa, likidhaminiwa na kampuni moja ya ulimbwende kutoka Ufaransa.
Pamoja na kujishindia taji,mshindi angepata kandarasi ya kuchapishwa kwenye jalida maarufu kule Ufaransa na pia kushirikishwa katika video za matangazo ya kibiashara na kampuni hiyo.
Marie alivutiwa na kuimezea mate kwani ingekuwa nafasi yake ya kipekee kujitoza kwenye jukwaa la kimataifa.
Manufaa yalikuwa ni mengi.
"Kama unapendezwa ningetaka kukusajili katika Mukta beauty designers and pagents" Muktar alimtupia wavu ili kumnasa.
"This is a dream come true!Bila shaka nimekubali" Marie aliitikia huku akijipepetea upepo kwa kutumia mikono yake kutokana na msisimko.
"Great nakuomba sasa twende katika chumba cha kibinafsi tukatikie kandarasi sahihi"
"Bila shaka,after you" Marie alikubali huku akiinuka.
Muktar alimwongoza hadi kwenye chumba kilichokuwa pembeni mwa orofa ya nne.
Muktar alifungua sefu yake na kuyatoa makaratasi ya kandarasi na kumpa Marie kusoma na kutia sahihi.
"Natumai tutakuwa na sherehe hapa baada ya kutia sahihi" Muktar alisema huku akikonyeza jicho moja na kutapatapa kitandani.
Marie hakusema lolote kwani alikuwa amezama kuyasoma yaliyoandikwa.
"Nimesoma na kue..." Marie alikatizwa na kugongwa kwa mlango.
Muktar alishtuka kwani hakuwa akimtarajia yeyote.
Kabla ya kuinuka kuangalia nani alikuwa mlangoni, Nyundo na Mubabe walijitoza ndani.
"Oh meet my manager and my  Lawyer" Marie alisema kuwatambulisha babake na Nyundo.
Hamaki zilimpanda Muktar akajiona kama paka aliyechezwa na panya.
Mubabe aliichukua kandarasi ile na kuisoma kabla ya kuitia sahihi na kumpa Marie kufanya vile vile.
Pumzi zilikuwa zinamtoka Muktar kwa kasi na kijasho chembamba kumbubujika makwapani.
"I think we are done now,we keep our copy"
"Tutazidi kuwasiliana kabla ya mashindano ili kujiandaa" Marie alimwambia huku akiwaongoza wenzake kutoka nje.
"Ok,sa...sawa!" Muktar aliilazimisha miguu yake kusimama ili kuwaaga.
Baada ya watatu hao kuondoka, Muktar alijirusha kitandani huku akijiuma kidole kwa kufeli katika mtego wake.
Baada ya wiki tatu shindano likifanyika na Marie akachukua nafasi ya pili.
Ila hakushiriki kama mshiriki chini ya Muktar.
Aliamua kuivunja kandarasi na kushiriki kama mshiriki wa kujitegemea.
Aliyeshida alikuwa ni mwigizaji chini ya Muktar.
Kwa kutumia ushawishi wake, Muktar aliweza kumpiku Marie na kuamua mshindi.
Wengi waliotizama walianzisha mijadala katika mitandao ya kijamii wakiteta kuwa aliyeshida hakuwa na uwezo wa kuafiki hata nafasi ya kumi.
Marie alipata uungwaji mkono katika mitandao ya kijamii,jambo liloelekea kampuni mdhamini kuvunja uhusiano na Muktar na kutia kandarasi na Marie.
Ama kweli bidii ya mchwa haiondoi kudura.
Mtoto 'Marie designers and beauty agency' akazaliwa na kutambaa kwa wakati mmoja.

SUZANNAWhere stories live. Discover now